VITA YA DUNIA DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA:Tuiache Mamlaka Ifanye Kazi

Posted: February 15, 2017 in Uncategorized

Madawa ya kulevya leo ni moja ya matatizo makubwa yanayosumbua karibu nchi zote duniani ikiwa ni pamoja na Tanzania. Matokeo ya madawa za kulevya aina hiyo, uraibu, ulanguzi au hata ulimaji inaweza kuleta; athari kubwa na kwa bahati mbaya vijana wanaathirika zaidi juu ya dawa za kulevya na hii huleta athari kubwa na mbaya kwa jamii.

Cha kusikitisha, madhara ya madawa ya kulevya nayaona katika nyanja mbalimbali. Watu wanaotumia dawa za kulevya wanakumbana na madhara ya kimwili kutokana na madawa hayo ya kulevya. Watumiaji wengi wa madawa ya kulevya kushiriki katika vitendo vya kihalifu, kama vile wizi na ukahaba ili kupata fedha za kununua dawa hizo, na baadhi ya dawa zinahusishwa na tabia za vurugu. Madawa ya kulevya husababisha utegemezi wa kisaikolojia na utegemezi wa kiuchumi. Matumizi ya madawa muda mrefu ni kiashiria cha kujichimbia kaburi bila kujali kama wewe binafsi ni tegemezi, kwa ujumla watumiaji wengi ni wachanga katika kufikiri, wanaosumbuliwa na hali ya hatari kiafya, kiakili, kimwili na kihisia kusumbuliwa kunakotokana na asili.

Zaidi masuala binafsi ya afya, zaidi ya madhara makubwa kwa familia, zaidi ya takwimu za uhalifu katika jamii, madawa ya kulevya yana athari kubwa katika uchumi wa Tanzania. Kusema kweli Mamlaka ya Kuzia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), wataalam katika matibabu na watunga sera, Mashirika binasfi n.k nadhani ni dhahiri wataunga mkono hoja yangu juu ya athari mbaya za madawa ya kulevya katika kujenga uchumi wa Tanzania. Hii ni pamoja na gharama za utekelezaji wa sheria, kufungwa jela, matibabu, majeruhi yanayotokana na ubebaji au majeraha yanayotokana na ajali za barabarani, wanaopotea wakiwa katika sehemu za kazi, n.k. Tukiweka baadhi ya mambo pamoja yanayohusiana na pombe na madawa ya kulevya utaona vifo vinavyoongezeka miaka hadi miaka, na hatari kubwa ya maambukizi ya VVU kwa kutumia sindano zinavyozidi kupukutisha jamii. Ukiachana na vifo katika familia zetu mtumiaji ambaye ameishazoea madawa ya kulevya kwa kawaida ni ngumu kubadilika kitu ambacho kina uwezekano wa kusababisha matatizo ya ndoa na kutokua na mahudhurio mazuri kazini na kujikuta akishuka utendaji wake na kupelekea kuachishwa kazi. Madawa ya kulevya yanaweza kuharibu maisha ya familia na kujenga mifumo ya uharibifu ya ushirikiano tegemezi; tatizo hili ni kubwa sana na linaweza hatimaye kuzuia maendeleo katika jamii.

Ingawa katika jitihada zinazoendea kufanywa na serikali imedhamiria kupunguza kasi ya makosa yanayohusishwa na dawa za kulevya Tanzania, ikiwa ni kuongeza mapambano dhidi ya matumizi ya madawa ya kulevya na usafirishaji wa madawa hayo kadri itakavyowezekana kama ilivyotajwa hivi karibuni na Rais Daktari Magufuli wakati akimuapisha Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya Bwana Rogers Siyanga.

Mara nyingi, baadhi ya wasafiri wamekuwa wanakamatwa katika viwanja vya ndege vya kimataifa au bandari na mizigo mikubwa ya mihadarati, hasa cocaine au heroine. Lakini licha ya ukamataji mkubwa wa wahusika na washukiwa mbalimbali, biashara ya madawa imeendelea kushamiri, hasa hapa nyumbani (Tanzania) hutumika kama kituo cha usambazaji kupitishia biashara ya madawa kimataifa. Moja ya sababu za kwa nini biashara hii iliendelea kushamiri ni ukosefu wa jitihada za dhati kutumia chombo kilichoundwa kwa mujibu wa taratibu na sheria lakini kikawa hakifanyi kazi japo kimekuwa kikitengewa fedha kwenye bajeti zetu kwa ajili ya kutekeleza majukumu yake, pamoja na bidii kubwa ikihitajika kwa upande wa wakala wote na mahakama kuwafungulia mashitaka wahalifu pale wanapokuwa na ushahidi wa kujitosheleza. Naamini kuwa na haraka na kwa bidii wahalifu kushitakiwa kwa kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya kwa njia yoyote kama unao ushahidi idadi ya kesi itapungua na haki kutendeka.

Aidha Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, bado wanaweza kuendelea na tempo (kama alivyoeleza Bwana Kamishna Mkuu wakati wa Awamu ya Tatu ya RC Makonda) ya ufanisi wake kwa kuwekeza zaidi kwenye vifaa vya teknolojia ambavyo vinaweza kuongeza uwezo wake wa kuchunguza wafanyabiashara au watumiaji kuzuia na kukatisha tamaa jitihada zao. Kutokana na uharibifu mkubwa unaosababishwa na mihadarati kwa jamii, hakuna jitihada za lazima zitakazoachwa na serikali yoyote makini kukabiliana na hatari yake. Njia nyingine ya kuhakikisha Mamlaka inafanikiwa katika malengo yake ni kuhakikisha kuwa mkuu wa shirika lazima arejeshe vijana kujitambua na jamii itambue madhara ya dawa hizo, na njia zinazoweza kutumika ni kutangaza kampeni dhidi ya biashara ya madawa ya kulevya. Watu wapate mafunzo ya kutosha ili kujenga uzoefu na utaalamu. Zaidi mamlaka inaweza kuongeza hamasa ya vita dhidi ya biashara haramu ya dawa tajwa inayofanywa na kupiga vita uendelevu wake kwa kuelimisha umma kwa kutumia mbao za matangazo, radio, televishen, vipeperushi, nk, yote yalenge katika jitihada za kuonyesha hatari ya madawa ya kulevya. Napendekeza pia kuanzishwa kampeni dhidi ya matumizi ya madawa katika mitaala ya shule za sekondari pia wanapaswa kuwajulisha vijana haja ya kujua kwa undani kasumba na ujumbe wa kupambana na madawa ya kulevya. Hii ni vita dhahiri ambayo jamii ya Watanzania hawawezi kumudu kupoteza, inauimiza moyo zaidi kusikia kwamba kuna tani za madawa ya kulevya katika mzunguko ambao ni dhahiri unalenga kumaliza jamii ya vijana wengi.

Karibu kila siku katika vyombo vya habari ni vijana wa Kitanzania ambao wanakamatwa wakati wa majaribio ya kusafirisha madawa ya kulevya kama cocaine na heroin ndani na nje ya nchi. Inafikia sehemu ambayo ukijitambulisha kama Mtanzania unaona kama na wewe utahisiwa kuwa mmoja wa vijana wanaotumia, wanaosafirisha au wanaofanya biashara ya dawa za kulevya. Vijana wameharibu sura ya Taifa iliyojengwa kwa muda mrefu na kwa gharama kubwa.

Umoja wa Mataifa Ofisi inayoshughulikia Madawa ya Kulevya na Uhalifu (UNODC) iliwahi kufafanua madawa ya kulevya kama biashara haramu ya kimataifa ambayo inahusika na ulimaji, utengenezaji, usambazaji na uuzaji wa vitu ambavyo vimekatazwa chini ya sheria ya dawa za kulevya.

Asili ya matatizo ya dawa za kulevya Tanzania inasemekana chanzo chake ni kipindi tu baada ya Vita Kuu ya Pili. Askari wetu aliyekuwa akihudumu huko Burma, India, alirudi na mbegu za mimea ya bangi. Askari huyo alikwenda mbele zaidi akafanya majaribio la kupanda mbegu yake na kugundua kwamba ilikuwa imefanya vizuri sana katika baadhi ya maeneo ya Tanzania, na hii ilisababisha kupamba moto kwa kilimo cha mmea huo.

Ilikuwa ni suala la muda tu na uwezo kabla wa idadi ya biashara ya mmea huo kuwa juu, baada ya kuboresha uchumi na kuongezeka kwa mfumo wa usafiri wa anga ikawa nafasi nzuri kwa vijana wachache wa Kitanzania ambao walikua na uwezo wa kujua masoko ambapo madawa ya kulevya wanaweza kuzalishwa na kusambazwa.

Kadri miaka ilivyoenda, Tanzania akawa msafirishaji na kituo muhimu cha usambazaji wa uhakika kwa cocaine, heroin na vitu vingine haramu lengo kwa ajili ya Ulaya, Asia ya Mashariki na masoko ya Amerika ya Kaskazini. Madawa yanayosafirishwa kwa wingi ni cocaine, heroin, bangi na mirungi. Ila kwa hapa nyumbani watu wengi sana wanasafirisha bangi ikiwa katika hali yake ya mitishamba kwa sababu ni nafuu kabisa na ni rahisi kutokana na ukweli kwamba ni zao linalolimwa na linazalishwa ndani ya nchi.

Mihadarati ni kawaida kusafirishwa kinyemela kuvuka ardhi, anga na bandari za bahari na maziwa yetu. Wale wanaosafirisha kinyemela kwa njia ya anga ni kawaida kwao kuonekana kama wafungwa katika filamu na kukata tamaa, kwa kuwa hawana uhakika wa kufika safari waliyotumwa au wanayoenda kuifanya wenyewe au wataishia mikononi mwa mikono ya dola.

MAMBO yanayofanya vijana kujiingiza kwenye biashara ya dawa za kulevya.

Watu wako tayari kuchukua tahadhari kubwa ya kuendeleza biashara za madawa ya kulevya lakini wanaangalia katika nchi kama Tanzania yenye mizigo mingi ikiwa ni pamoja na uhaba wa ajira, umaskini, rushwa na hasara ya jumla ya matumaini katika serikali, vinakwanza na kuona njia pekee ya kujitengenezea pesa ni katika biashara hiyo haramu lakini wafanyaje?

Sababu nyingine ni jitihada ya vijana wengi kuhitaji fedha nyingi na ya haraka bila kua na mpango unaoeleweka. Biashara ya madawa ingawa kwa ni hatari kwa muhusika lakini ni njia ya haraka ya kupata fedha. Vijana dhaifu ambao hawakuwa na mundo mzuri wa maadili kwa urahisi hujikuta wanaangukia kwenye uovu huu.

Nitumie fursa hii kulipongeza Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  kwa ushirikiano mlioonyesha kwa pamoja kupinga ukiukwaji wa sheria uliokua ukifanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bwana Makonda. Nchi yetu ilijengwa kwa amani kwa sababu ya sheria, taratibu na kanuni mbalimbali zinazotungwa, tukiacha kila mtu kufanya anavyojisikia hatuwezi kufika tunapopataka.

Twitter: @noor_abdul

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s