PONGEZI KWA DK. MAGUFULI NA MAMBO YA KUZINGATIA!

Posted: November 5, 2015 in Uncategorized

Mheshimiwa Rais, tafadhali niruhusu kuanza kwa kukupongeza wewe kuapishwa kama Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania. Mheshimiwa, imekuwa safari ndefu sana na ngumu kuelekea Ikulu; dhamira ulikuwa nayo na umethibitisha kwa ufasaha maneno kuwa “kamwe usichoke hadi uhakikishe unatimiza kile unachokusudia”. Kuna somo la kujifunza kutokana na uamuzi wako, mshikamano wako, uvumilivu mkubwa uliouonyesha katika kipindi chote cha kabla na baada ya uchaguzi.

Sasa kwa kuwa Mheshimiwa uko katika madaraka, ni wakati wa kukaa chini haraka na serikali hasa ya watu maridadi na makini katika kuunda Serikali makini. Siyo kwamba Watanzania ni wagumu sana kuongozwa lakini ukweli ni kwamba matarajio ya Watanzania ni makubwa baada ya kuugua/kuteseka kwa muda mrefu. Watanzania wa wastani wamekuchagua kwa kwa matumaini kwamba una uwezo wa kuwaondolea umaskini na kuwaweka katika ramani ya mafanikio. Hiyo imetokana na vilio na kelele za mabadiliko zilizokuwa kubwa sana na kufikiwa kutozuilika! Natambua ukubwa wa mzigo utakaoubeba kuanzia leo kwamba hakuna mtu anapaswa kuingilia.

Watanzania na dunia kwa ujumla, itakuwa makini kuangalia na kuchambua matendo yako ikiwa ni pamoja na lugha ya mwili wako kuanzia sasa na kuendelea. Uwezo wako mkubwa wa kuongoza utakuwa ni jinsi ya kusimamia wanasiasa wakaidi ambao watataka mazingira yetu ya kisiasa yaendelee kuwa katika mifumo waliyoijenga wao. Kwa wale wachache naamini wataifanya kazi yako kuwa ngumu zaidi kwa sababu naamini mifumo iliyoshindwa itatoa sababu na vikwazo vya kukwamisha mabadiliko mapya maana wengi wao si kweli kuwa wanaamini katika kanuni/misingi na itikadi zako. Ajenda yao haiwezi kuwa na uwezekano madhubuti juu ya uendeshaji wa nchi. Naamini wao wana wasiwasi, pia hawaamini kwamba utakuwa na muelekeo mpya wa kutatua na kuondoa rushwa kwa maono yako na taifa likabaki la watu wasafi. Kama utatimiza ahadi zako kwa wananchi, naamini mambo mabaya hayatakupata utakuwa na wakati mzuri wa kusherehekea na wananchi waliokupatia ridhaa. Lakini kama utashindwa, wanasiasa walewale ambao wamekupatia ridhaa ya kuwaongoza watakuadhibu kwa kutumia sanduku la kura hilo hilo na utakuwa umewapa nafasi na hoja juu ya kushindwa kwako na kuonyesha kuwa tunarudi kwenye “business as usual”.

Sitarajii na kama ilivyo kwa Watanzania walio wengi, ikiwa ni pamoja na mimi mwenyewe kushindwa wanakuombea ufanikiwe. Katika yote naamini huwa yanatokea yasiyotarajiwa, na matumaini yetu ni ushindi tena kwa nyanja nyingi, najaribu kuona kuwa wewe ni mtu wa mwisho utakayezima taa za matumaini ya watanzania kote nchini na hasa vijana ambao ukishindwa utawarudisha katika giza la milele. Wewe ni mwenge wa matumaini ya kushikilia kwa Watanzania wa nyumbani na nje ya nchi. Mengine yanabaki kuwa historia, imetuchukua miaka mingi ya majuto kabla ya kuwasili katika wakati huu na hatuwezi kumudu kuendelea kupoteza muda mwingine. Mzigo wa matarajio juu yako na Makamu wako Mama Samia, ni mkubwa na mzito.

Mtihani wako wa kwanza ni jinsi gani utateua timu ya “mabadiliko” inayotarajiwa sana na kwa shauku. Hakika lazima kutangaza baadhi ya teuzi muhimu mara moja ili zile siku mia moja ziwe za ufanisi. Baadhi ya majimbo tayari yamepata wa kuyaongoza na hii inaonyesha ishara ya maandalizi ya kupokea mabadiliko. Serikali mpya lazima ichote uzoefu kutoka kwa watu ambao wamewahi kutumikia nchi hii katika nafasi za juu za uongozi.

Mheshimiwa Rais, katika teuzi zako rushwa isipewe nafasi lazima ufanye kila kitu muhimu kwa kuchagua baadhi ya wanaume na wanawake wenye uwezo wa kuongoza waliobarikiwa kwa vipawa vya kuongoza toka kwa Mungu na hiyo itakuwa ni zawadi kubwa kwa Watanzania. Kama tayari zimefanyika teuzi hizo tafadhali nashauri kutangazwa kwa wahusika kama jambo la dharura. Katika teuzi za kisasa tawala za serikali zinaongozwa na uwazi na si za kufunikwa na usiri. Hiyo ilikuwa ni moja ya mapungufu ya utawala uliotangulia, ambayo nakushauri Mheshimiwa Rais usifanye makosa hayo. Seti ya kwanza ya uteuzi wanaweza kufanya au kunyongonyeza serikali hii hasa kama ni wale wanasiasa waliojengwa kwenye misingi ya kujuana na teuzi za makundi ya kulipa fadhila. Kwa kweli, ni vigumu kupuuza kila tetesi za chama fulani kwa sababu ya kutopata ridhaa ya kuongoza zinazotolewa kwenye majukwaa kwa kuweka tetesi hizo katika makapu ya kutozifanyia kazi kuona zina ukweli kiasi gani. Lakini pia ni jinsi gani ya kudumisha ushirikiano na kuonyesha wazi kama ni kwenda kuwa biashara kama kawaida katika Tanzania au vinginevyo.

Mheshimiwa Rais, napenda kukujulisha kuwa macho na vyombo vya habari ikiwa ni pamoja na jeshi la vijana wasiokuwa na ajira na kushinda kwenye mitandao ya kijamii wakivuruga misingi na taratibu za vyombo vya habari. Vyombo vya habari havina malengo hasa ya kuanzishwa kwake, tena baadhi vikiwemo vya waandishi wa habari wakubwa lakini pia wachapishaji binafsi maalumu na wanablogu juu ya jamii wamepoteza maana halisi ya vyombo vya habari zaidi wamekuwa ni sehemu ya kusemana, kuchonganisha na kutoa tuhuma zisizo na chembe ya ukweli. Wamekuwa hawawezi kusikiliza kwa makini na kukwepa shida ambayo wanaweza kuleta ndani ya jamii. Timu yako ya vyombo vya habari lazima ijenge misingi imara kutoka mwanzo. Kama wako watu ambao misingi ya vyombo vya habari hawaitambui au hawana ushawishi ndani ya wanahabari, na hawawezi kujenga hoja kwenye majukumu yao wanaweza kuyeyusha ndoto na matumaini ya watanzania. Ni lazima iwe wazi kwamba kuwepo tofauti kati ya waandishi wa hotuba zako na wale wanaoeneza sura ya utawala wako. Wakati watangulizi wako wanaweza kuwa karibu na wewe na labda ni rafiki zako, mwisho wa siku hawana jipya. Kinachotakiwa kwa ajili ya mwisho ni wale ambao wanaweza kuungana si tu kwa mtandao wao lakini pia kwa uraia wa nchi hii.

CCM imedumu madarakani kwa miaka 38 lakini jumla ikitawala kwa zaidi ya nusu karne wakiwa katika mwavuli wa TANU. Watu mitaani wana njaa na kiu ya mabadiliko. Serikali yako inategemewa kutoa huduma bora na si propaganda ambazo wananchi wanaweza kufikiri kuwa kusema uongo ndio njia ya kushinda mioyo na roho za watu. Tanzania yako (kama unavyopenda kusema) iwe ya kisasa zaidi kuliko kurudishwa nyuma wakati walipokuwa na watetezi wa serikali waliozoea kutusi akili zao bila woga na manyanyaso.

Baraza lako la mawaziri linapaswa kuwa makini na lililojipanga kwa nia ya kujenga Tanzania mpya. Watanzania kwa pamoja tumechoshwa na misaada wakati tuna rasilimali zenye uwezo wa kutukomboa! Una taifa la zaidi ya watu milioni 45 wasomi wazuri na wenye ueledi naamini haitakuwa kazi nzito kutafuta na kubaini wachache wa kusaidia serikali yako kufikia malengo makubwa. Kuna kazi nyingine nyingi kwa watakaokabidhiwa nyadhifa lakini roho ya serikali yoyote ni baraza la mawaziri. Mawaziri ni Mabalozi wa serikali yako. Wao lazima wapimwe na kuaminiwa na ambao wanaweza kuheshimiwa na kuhamasisha Watanzania katika hali ya sasa ya kukata tamaa. Ni lazima wawe watu waliojipanga kutimiza matakwa ya utawala wako, maono yako na malengo yako. Baraza lako la mawaziri liundwe na wanaume na wanawake ambao wewe binafsi utajisikia furaha kufanya nao kazi bila kua na wasiwasi nao.

Kuna maeneo muhimu ya kipaumbele. Kinachounganisha watu kwa kila familia katika nchi yoyote ni ELIMU. ELIMU Ni msingi wa mafanikio au kushindwa. Kama tunaweza kuokoa elimu yetu haraka lazima tujenge mazingira bora ya sekta ya elimu. Katika siku za nyuma, wengi wetu tulihudhuria Shule nchini na wachache walisafiri nje ya nchi. Uwekezaji katika elimu ya nyumbani ni muhimu sana maana tutakuwa tunazalisha ajira kwa watu wetu na tutajenga jamii bora. Ujinga ni mama wa yote. Hakuna taifa linaloweza kupiga hatua za maendeleo ikiwa wananchi wanaishi katika ujinga uliokithiri.

Mheshimiwa Rais, uchumi wetu ni wazi hauko katika hali nzuri. Kama Mzee wangu Kingunge anavyopenda kusema “ndani ya miaka kumi tumekuwa tunaenda mbele na kurudi nyuma”. Tumejenga utegemezi kwa wahisani ambao tumefikia hadi kwenye bajeti ya Taifa tunasikia asilimia kadhaa inategemea wahisani. Katika uongozi wako ni matumaini yangu kuwa hali hii itaondoka maana kumtegemea mtu ambaye huna uhakika nae ni ishara ya kuanguka kifikra, naamini pia miaka kadhaa ijayo tutaanza kunufaika na mapato ya gesi, madini na rasilimali zingine kwa kuweka utaratibu mpya wa kuhakikisha keki ya Taifa inanufaisha kila mmoja wetu. Kilimo ni moja ya sekta muhim sana hapa nchini hii, na namshukuru Mungu tumekuwa tukishiriki kikamilifu katika kilimo japo kuna changamoto nyingi za wakulima ikiwemo kubwa ya serikali kukopa mazao na kucheleweshewa malipo na moja kwa moja kuwafanya waishi katika maisha ya shida. Wakati nakua niliamini kilimo ndio ilikuwa suruhisho na kwa bahati matajiri waliokuwa karibu walikuwa wakulima wa kahawa na Pamba. Lakini wao kwa sasa ukiwasikiliza wana vilio vikubwa juu ya mazao yao waliyokopwa na Serikali. Hiyo ni aibu kubwa kwa serikali. Imefikia hatua ambayo watu wanaanza kuoanisha methali na maisha ya serikali kwa watu wao. Mkulima mmoja aliwahi kuniambia wakati anasoma miaka ya 60 aliambiwa “Mtu mwenye mkono mrefu ni mwizi” na mara nyingi Serikali imekuwa ikijipambanua kwa kusema ina mkono mrefu, Je ndio inahitimisha maana halisi ya ile methali? Mheshimiwa Rais tunapaswa kurudi katika hali ya kawaida kama zamani ambapo serikali iliheshimika.

Mheshimiwa Rais tasnia ya burudani kwa sasa ni biashara na wanafanya vizuri kimataifa. Wakati umefika kusimamia vizuri sekta hii kwa namna ambayo italeta mavuno mengi kwa vijana wenye vipawa. Wanaweza kutengeneza mamilioni iwapo watawekewa mazingira ya kujiajiri kama waimbaji, wazalishaji, wahandisi, mameneja matukio, wabunifu, mafundi, Deejays, wachekeshaji, choreographers, Watunzi, wapambaji, na kadhalika, kama wataweza kusimamiwa vizuri na kuelekezwa katika mwelekeo sahihi na serikali yako, naamini Watanzania wana vipaji vya kweli katika michezo lakini hawajawezeshwa vya kutosha.

Kila Mtanzania, tajiri au maskini, amechanganyikiwa kuhusu kukatika kwa umeme japo kwa sasa kwa wiki hizi mbili kuna unafuu. Hakuna kitu kikubwa zaidi kuliko kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa aibu hii ya kitaifa. Kama Utafanikiwa kutatua hilo, Watanzania watashukuru milele. Toka nimezaliwa naambiwa Bonge la Stiglers Gorge lina uwezo wa kuzalisha umeme wa kutosha kulisha nchi nzima na kubaki na ziada, najiuliza kwa nini isiombwe hela kwenye taasisi kubwa za fedha kama Benki ya Dunia au Shirika la Fedha Duniani ili wakatatua hilo tatizo? Nikiwaza kilichotokea kwenye maeneo ya madini nazidi kujiuliza kama tutakuwa na usimamizi wenye tija na uwazi katika sekta ya gesi kama si kuturudisha kwenye tawala iliyopita.

Mwisho naamini kwamba Serikali yako lazima ikabiliane na viashiria vya ukosefu wa amani mara moja katika nchi yetu. Utaongoza serikali yenye usawa na ndugu zetu wenye albinism wapewe heshima na nafasi kama wanajamii wengine.

Kwa mara nyingine tena, naungana na watanzania wengine kukupongeza. Mheshimiwa Rais nakuombea mafanikio katika kuleta matumaini na mabadiliko katika nchi hii!

Mungu awabariki,

Mungu ibariki Tanzania,

Mungu ibariki Afrika.

Abdul Noor,

Twitter: @noor_abdul

Instagram: @abdul_noor

Facebook Page: Abdul Noor

Email: abdulnoor3@gmail.com

www.abdulnoorblog.wordpress.com

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s