Demokrasia Inapofinywa!

Posted: November 4, 2015 in Uncategorized
Tags: , , , ,

Naomba tusikilizane watu wangu, kama mtu yeyote atapenda au la, kama niko sahihi kisiasa au la, maneno haya yamekuja mawazoni mwangu: mahitaji ya wengi yanazidi maslahi ya wachache. Yanajitosheleza, yana usugu, yana tahadhari, na naamini kuwa uongozi wa Taifa hili la Tanzania umetekwa nyara na watu wamezoea kuhodhi madaraka bila ya kuyapigania kwa njia ya kidemokrasia. Aibu ya Tanzania ni kutokua na uimara wa wasomi wa kisiasa ambao mara kwa mara wameshindwa kufuata kanuni za misingi ya demokrasia. Upendeleo huu wa kutisha umekuwa daraja kubwa zaidi kwa kuongezeka uzoefu wakupeana madaraka wakiamini wao ndio wenye haki ya kutawala na kufifisha ndoto za kidemokrasia nchini mwetu. Leo hii, Taifa la Tanzania kama vile mataifa mengine dhalimu wa madaraka linajikita katika kitovu cha kukandamiza demokrasia iliyoonekana walau inaanza kukua japo katika hali halisi inakuwa kwa kutamkwa tu si katika hali halisi. Hii inanifanya nione kuwa wanaoitwa waangalizi wa kimataifa si lolote si chochote zaidi ya kuwaita watalii na kusababisha mataifa yaliyowatuma kuonekana ni sehemu ya kudhoofisha demokrasia na kuwajenga watu katika nyuso za kukata tamaa. Watanzania siamini kama bado ni wa kuuzwa kwa bei ndogo kiasi hiki, hawawezi kufanyiwa mazingaombwe ili kuwasaidia kupata kiongozi wa kuwavusha katika mateso ya sasa yasiyoendana na umri wa Taifa hili toka kupata uhuru, familia zinaishi kwa shida hasa za vijijini ikiwa ni zaidi ya mateso na matumaini yakiwa kwamba siku moja mabadiliko yatakuja. Nina bidii kuangalia katika nyoyo za watu wanaotafuta madaraka, na nina majuto moyoni kuwajulisha Watanzania kwamba mkombozi bado hajafika. Ni lazima wakaze wenyewe kwa ajili ya mabaya yanayokuja, ugumu wa maisha utachukua nafasi kubwa nchini, na matajiri wataendelea kuwa matajiri katika kila hali, lakini pia maskini wataendelea kuwa maskini zaidi ya sasa. Hadi wakati huo ambapo tutavuna tulichopanda kulinda heshima na utukufu wa jamhuri yetu. Hivyo basi tutaangalia mienendo ya kuwakaribisha watawala wapya kukiwa hakuna tumaini lolote la kupata Taifa jipya ambalo kutasababisha kuwepo kwa huruma, kujituma, uongozi makini, matumaini, uaminifu na juu ya yote, upendo kwa wote. Katika uchaguzi huu, mshindi amepatikana lakini si kwa mapenzi ya waliowengi au niseme si chaguo la walio wengi ni njama za chama kilichoshika hatamu kuendelea kutawala kwa mabavu na kufifisha demokrasia, lakini naamini, amekuja kuandaa njia kwa upinzania kwa ajili uchaguzi ujao japo safari ni ndefu.  Tanzania ni kubwa lakini kabla ya hapo, atatakiwa kuwajengea Watanzania moyo wa uaminifu kuwa yeye atakuwa tofauti na mtangulizi wake lakini pia kutegemea imani yake, kwani imani bila matendo ni bure.

Mungu Ibariki Tanzania.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s