KWA NINI WATU HUSEMA UONGO?

Posted: March 2, 2015 in Uncategorized

Natumai wote mnaendelea vizuri katika mfungo huu wa kwarezma.

Ujumbe wangu kwa leo, unahusu “kwa nini baadhi ya watu husema uongo?”

Uongo mfumo wake, una msingi wa kwenda kinyume katika matendo na maneno. Mara nyingi, baadhi ya binadamu wanachukia kuambiwa au kusema uongo, lakini kwa upande mwingine, hujikuta wakitumia uongo kama kinga ya kuendeleza mfumo wa uhusiano husika. Ninaposema mfumo wa uhusiano, namanisha kulinda maslahi ya nafsi zako.

Licha ya kila nafsi kuchukia kuambiwa uongo, kuna siku ambayo nafsi hiyo yenye kuchukia uongo, nayo hujikuta katika njia yenye matumizi ya uongo, moja wapo ya njia ya kujihami au kutengeneza mazingira ya kupata jambo fulani kutoka sehemu fulani.

Kwa mfano:

Uhusiano wa mwanamke na mwanaume (boyfriend or girlfriend).

kwa utafiti uliofanywa na blog hii juu ya mahusiano unaonesha kwamba asilimia tisini (90%) ya uhusiano wa vijana wenye umri kuanzia miaka 12 hadi 35 wa jinsia zote (wanaume na wanawake), hujikuta katika uhusiano wenye msingi wa penzi la uongo. Msingi wa penzi la uongo una maana gani?

Maana ya uhusiano wenye msingi wa penzi la uongo ni kumdanganya mwanamke au mwanaume, ili aweze kukupenda. Wanaume wanabeba asilimia themanini (80%) katika uhusiano wa mbinu ya uongo na wanawake wanabeba asilimia 20%.

Wanaume wana mfumo wa kutumia mbinu za kulaghai kupitia miliki (magari, nyumba, pesa ya msimu, mavazi ya kuazima, maneno mazuri na yenye vionjo vingi vya kujenga imani ya mwanamke…..n.k). Mwanaume huchukuwa nafasi hii, kwa kumshawishi mwanamke, na kujenga msingi wa kulazimisha penzi ndani ya moyo wa mwanamke, kupitia njia ya vishawishi vya matendo na maneno. Mwanamke mwenye upungufu au mahitaji ya fedha, hujikuta katika mtego wa vishawishi vya mwanaume. Mara nyingine kuna wanawake wenye hifadhi ya tamaa ndani ya nyoyo zao, hawa huwa ni rahisi kujikuta katika mtego huo. Kwa sababu wanapenda kuonekana katika jamii wakila au kutembelea sehemu za kifahari na mara nyingine wanawake hao, huwa ni wenye tamaa ya kuvaa au kumiliki vifaa vya mawasiliano vyenye bei kubwa na mara nyingine hujikuta wakihitaji kuishi katika nyumba za kupanga ambazo ni nzuri, na kumbuka kwamba uzuri wa nyumba ndio ukubwa wa gharama ya kodi na uendeshaji (umeme, maji, kulipa mfanyakazi….n.k). Hayo yote ni baadhi ya mambo ambayo yanamvutia mwanamke mwenye tamaa ya mali. Njia hii ya mwanaume kutumia pesa au mali yake kumshawishi mwanamke au wasichana wadogo na wengi wao wakiwa ni wenye ukosefu au kipato cha chini, huwa ni yenye kusababisha magonjwa ya zinaa ikiwemo UKIMWI au kupata mimba zisizotarajiwa na njia hii huondoa heshima ya familia au ukoo fulani. Vile vile njia hii, humtegenezea msichana husika, kushindwa kupata ulinzi wa ngono, kwa sababu anapotoswa, huwa ni mwenye kuongeza idadi ya wanaume, ili apate matumizi yake na matunzo ya mwanae (kama alipata mtoto).

Kwa upande wa vishawishi vya uongo kutoka kwa mwanamke kuelekea kwa mwanaume, huwa ni vyenye (vishawishi) nguvu na vyenye kupendeza katika mda muafaka. Kwa sababu, mwanaume anategemea nguvu na akili yake, ili aweze kufanikisha ndoto yake maishani. Mwanaume mwenye kukata tamaa, huwa ni mwenye roho mbaya na kufikia hatua ya kuweza kujitoa nafsi yake, kutokana na kushindwa kuendesha maisha yake. Mwanaume mwenye upungufu au ukosefu wa kipato, huwa ni mwenye kutawaliwa na udhaifu wa maamuzi.

Njia hii ya udhaifu, humpa mwanamke mwenye mahitaji ya penzi, ramani ya kumpata mwanaume huyo, bila hata ugumu wa majadiliano. Kwa sababu, kijana (mwanaume) huyo, yeye huona kama bahati iliomdondokea kutoka mbinguni. Kijana huyo kumshauri au kumuomba ajiepushe na vishawishi vya uongo vya mwanamke husika, huwa sio rahisi kwa sababu kijana atamuona mwanamke huyo ni mkombozi wa shida zake (chakula, mavazi, marazi, matibabu, nauli au kupewa usafiri, kupewa kiasi fulani cha pesa au mali……n.k) yote haya kijana huyo (mwanaume) alikuwa hawezi kuyapata katika jamii iliomzunguka, bali huona mwanamke huyo aliye jitokeza katika jamii, na kujali hisia zake zenye msingi wa taabu na maumivu hadi kufikia hatua ya kupoteza muelekeo wa maisha, ndie mtu mwenye thamani na umuhimu maishani mwake.

Njia hii huwa ndicho chanzo cha vijana wengi wenye kulelewa na shuga mami/shuga dadi, kuambukizwa magonjwa ya zinaa na mojawapo katika msingi wa magonjwa hayo ni ukimwi.

Katika kumalizia naomba kujua baadhi ya mambo.

Je unaweza kuchumbia hadi kupeleka mahari bila kujua unaemchumbia anatoka katika familia gani?

Advertisements
Comments
  1. thobias wolstani says:

    walo wengi hupenda tumia uwongo ili kutimiza malengo yao ususani pale wanapo kua nashida ya maitaji ya vitu kwa maitaji ya nafsi zao.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s