VALLENTINE LETTER!!!

Posted: February 13, 2014 in Uncategorized

VALLENTINE LETTER!!!

Sweetheart,

I have been greatly comforted by being informed that my sister –in-law and parents are supporting us in our avowed determination for the two of us to be wife and husband till death tears us asunder. Further that they have given the green light, so that the two of us may seriously put our thoughts together, be transparent on our planned course of getting married and ultimately plan the best way of performing the rituals of being formally introduced to your family members as is desired by our consuming love and in accordance with our cherished cultural traditions. Honey, I am most pleased in my heart for God’s guidance that enabled us to reach this stage.

Ila kitu cha msingi katika lengo letu lote ni sisi kwa pamoja na kwa nafsi ya kila mtu mmoja mmoja kati yetu, yaani mimi na wewe ni kujiuliza kwa kimoyo moyo na kwa ujasiri kuhusu tabia zetu zilikuwa ni za aina gani huko nyuma. Zilikuwa zimejengeka katika misingi ya upendo, uaminifu, maisha ya raha, uvumilivu na njema? Au ni zile ambazo zilitawaliwa na maovu na zikajipa matarajio ya mabadiliko ya kubadilika ndani ya ndoa?

Mimi huwa naamini kuwa ndoa ni mwendelezo wa tabia nzuri kwani maisha ya ndoa hayawezi kumbadilisha mtu kama hajaonyesha nia ya kubadilika. Maamuzi ya maisha ya ndoa kwa kiasi kikubwa hutegemeana na maamuzi ya wawili.

I have been, for sometimes now, thinking very deeply on our relationship and I have discerned your deep feelings of love towards me and I strongly feel that you are very likely the real one, the real wife that I have been missing throughout my life.

Ni vyema nawe pia ukafanya tathmini yako binafsi kuhusu mimi kwa kuzingatia malengo na matarajio yako ya maisha, uliyojiwekea na kuainisha kama mimi nimefuzu kuwa chaguo lako pekee la mume umtakaye maishani, kwenye maisha ambayo huwa hayatabiriki kwani yanaweza kuwa ya raha au kinyume chake.

Nasema haya yote, kutokana na uzoefu wangu kuhusu maisha ya mahusiano na ndoa kwa jamii ya dunia tunamoishi. Watu wengi hufunga ndoa kukidhi mchakato wa maisha tu. Ndoa za namna hii ni nyingi mno, na zimekuwa chanzo cha maangamizi ya duniani. Zimekuwa chimbuko la watoto wa mitaani, malaya, walevi wa kupindukia, kukosa dira na hatimaye kusababisha vifo vyenye machungu, lakini, naamini hali hii ingeweza kuepukika, iwapo jamii ya wanandoa wangefikia hatua ya kuoana kama hitajiko la moyo. Wakaongozwa na upendo, wakanuia kuaminiana, kuvumiliana kuheshimiana na kushauriana. Wakakwepa kabisa kuiga mila zisizo zao na wakaishi maisha ya uwazi na kuambizana ukweli. Maisha ya ndoa au mahusiano ya namna hiyo yanaweza kukidhi maana halisi ya ndoa ama mahusiano.
Kama tulivyowahi kuongea mara kadhaa, bila shaka ujio wako, umefungua ukurasa mpya wa maisha yetu ndani ya moyo wangu katika kipindi ambacho si kirefu. Natumaini mapenzi yetu yanalenga kufikia tunapopataka na hasa kuelimishana kuhusu mila na utamaduni wa kila mmoja wetu na mkakati wa kufanikisha azma yetu na si vinginevyo

Please I am requesting you to focus your attention to all the plans and suggestions that we have mutually been exchanging eversince we become tied up by our love bonds. May I also pay that showers, sparks and fires of true love radiate from your heart always.

Happy Valentine’s Day

Everlasting your loving husband,

Abdul

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s