Mahudhurio mabaya ya wabunge: Je wananchi wanawakilishwa ipasavyo?

Posted: April 11, 2013 in Uncategorized

Mahudhurio mabaya ya wabunge: Je wananchi wanawakilishwa ipasavyo?

WABUNGE wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanaendelea kupoteza umakini katika mahudhurio ya vikao vya Bunge na kusababisha hotuba ya bajeti ya Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki kusikilizwa na wabunge wasiozidi 36 wakati bunge letu hilo ambalo linapaswa kuwa na wabunge 357.
Wakati Mzee wa Kasi na Viwango (Mh. Samuel Sitta) akisoma hotuba yake, kambi ya upinzani ilikuwa na wabunge watano wa CUF, kumi wa CHADEMA, watatu wa NCCR-Mageuzi wakati CCM ilikuwa na wabunge wasiozidi 14.

Hapo ndipo najiuliza kulikua na maana gani ya kupanga kuanza vikao mapema na kuutangazia umma kuwa Bunge limefanya marekebisho ya baadhi ya mambo ndani ya bunge na kulifanya la kisasa? Au UTORO wa wabunge ndio mabadiliko yenyewe?

Nadhani kuna haja ya kufanya marekebisho ya kanuni mpya za mabadiliko ya Bunge, yaguse moja kwa moja kwa walengwa iwekwe kanuni ya utoro iwe moja wapo ya adhabu kwa wabunge aidha kwa kunyimwa posho ama kutoingia Bungeni kwa muda kadhaa ili kuimarisha nidhamu ya Bunge. Lakini wanazungumzia maslahi yao tu. Hakuna kanuni za Tija kwa Watanzania kama wawakilishi wao.

© Noor Abdul

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s