UPO KATIKA MAHUSIANO YA KIMAPENZI AMA MAHUSIANO YA KIMWILI NA MTU WAKO

Posted: April 9, 2013 in Uncategorized

UPO KATIKA MAHUSIANO YA KIMAPENZI AMA MAHUSIANO YA KIMWILI NA MTU WAKO

Wanadai hakuna awezaye kutoa maana halisi ya neno MAPENZI…eti kila mtu ayatafsiri anavyoweza…..….Siamini ila yawezekana….

LAKINI lipo jambo linanisumbua kichwa kiasi fulani…..hivi wewe kijana inakuwaje kila mara unapokutana na mpenzi wako mnaishia kufanya ngono kasha kila mtu anachukua hamsini zake? Hivi yawezekana kabisa hamna lolote la kuzungumza zaidi ya kufanya ngono? Yaani imekuwa mazoea hadi ukisikia mtu anamwambia mpenzi wake amemmis anakuwa anamaanisha ‘amemiss ngono’ hakuna jingine.

NDO najiuliza sasa hivi haya ni mahusiano ya kimapenzi ama ni mahusiano ya KIMWILI…..bila shaka ipo wazi haya yanakuwa mahusiano ya kimwili.…yaani wewe ukijua fika kuwa upo ‘periods’ tafadhali usije maana miili yetu haitapata nafasi ya kufurahishana…..

IFIKIE kipindi kama vijana tutambue kuwa mapenzi ni zaidi ya NGONO…mapenzi ni wigo mpana sana huenda ndo maana yakakosa changanuzi maalumu…….mpenzi wako ni zaidi ya rafiki na wakati mwingine ni zaidi ya ndugu…..basi mchukue walau dakika kadhaa kuzungumzia maisha kiujumla….

Ina maana nyie hamuwazi kuwa ipo siku mtaoana labda au mtakuwa na maisha yenu ya kujitegemea na kuzaa watoto? Kama mnayo mawazo haya na mnayazungumza basi mpo katika mahusiano ya kimapenzi lakini kama haya yanaishi katika ndoto zenu na kamwe hamyazungumzi bali mnavuana nguo kila leo basi mpo katika mahusiano ya kimwili. Inakuwaje nyie watu hamna hata mapumziko?? Hata Mbwa wenyewe huwa wana mapumziko……achilia mbali mbwa hata KUKU kuna kipindi jike linagoma kabisa ……sembuse wewe mwanadamu?????

MAHUSIANO ya kimwili ni hatari sana maana miili ikizoeana sana ile ladha ya siku ya kwanza inapotea…mwili unaanza kusaka ladha mpya…msichana anataka mwanaume anayeweza kwenda mizunguko mitano bila kupumzika….mwanaume naye anataka msichana mwenye nyonga pana na anayejua kuzitumia kitandani….

Utakuwa kwenye mahusiano ya KIMWILI hadi lini? Utabadili hiyo miili mpaka lini? Miili ipo mingi na inazaliwa kila leo…..ipo miili ya kila rangi…kila mvuto..ni wewe tu na uchanguzi wako….lakini katika kuibadili miili kumbuka ipo ambayo imetengenezwa kwa sumu kali…sumu ya gonjwa hatari jihadhari usije ukaambukizwa…..

ACHANA na mahusiano ya kimwili maana kamwe hutatimiza ndoto zako…jikite katika mahusiano ya KIMAPENZI….Uyatendee haki na mwisho wa siku utaitambua ladha ya mapenzi ilivyo tofauti na SHUBIRI ya mahusiano ya kimwili…….

WAPO wengine wanaweza kujenga hoja kuwa mahusiano ya kimwili husababisha mapenzi kuimarika…eti kisa tu miili inakutana….ingekuwa hivyo basio machangudoa wangeheshimika kwa kuzalisha mapenzi kila siku…..wako wapi sasa? Mbona hawaheshimiki? Mbona wanadharaulika……mwanamke ukiyapenda mahusiano ya kimwili basi WEWE NI CHOMBO CHA STAREHE na si mke mtarajiwa…..nawe mwanaume ukiyashabikia mahusiano haya itakuwia ngumu sana kudumu na mkeo…hasahasa pale utakapoizoea ladha yake…mbaya zaidi akishajifungua watoto kadhaa…….UTAZISAKA LADHA nyingine mpaka kero…..

JIBU lipo katika kichwa chako ni mara ngapi wewe na mwenzi wako mnazungumza kuhusu maisha ya sasa na baadaye? Ni mara ngapi mnatumi kutafakari mahusiano yenu na familia zenu kwa ujumla?….ni wewe sasa kutambua kama u katika mahusiano ya kimwili ama mahusiano ya kimapenzi……kama hapo ulipo ni sahihi kwako kamatilia hapo hapo…

#USILIFANYE penzi lako kama Profile Picture ya facebook…kila anayebofya jina lako anaiona…….yaani kila anayekutongoza we unakubali tu……HUJUI KUKATAA mwee!!

**Kama kawaida mtazamo wangu simlazimishi mtu kuuchukua lakini ukiona unakufaa wewe chukua tu……***

Advertisements
Comments
  1. mtoto wa mama marim says:

    nimeipena sana

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s